Friday, May 13, 2016

Mashambuliaji wa kiabu ya Paris St-Germain Zlatan Ibrahimovic ataondoka katika klabu hiyo mwishoni mwa msimu huu.
Kandarasi ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 34 inakamilika msimu huu na amehusishwa na uhamisho wa Manchester United,kilabu ya Los Angels Galaxy na AC Milan.
''Ninafurahia'',alisema.''Niliwasili kama mfalme na sasa naondoka kama kigogo lakini ntarudi''.
PSG imesema kuwa Ibrahimovic anaondoka kama mshambuliaji bora na mchezaji bora zaidi katika historia ya kilabu hiyo.
Ibrahimovic ameifungia mabao mengi zaidi klabu hiyo licha ya kujiunga nayo mwaka 2012 aiwa amefunga mabao 152 katika mechi 178.
PSG imeshinda taji la Ligue 1 kila msimu tangu Ibrahimovic ajiunge na kilabu hiyo.
.



Thursday, May 12, 2016

JE KIM KARDASHIAN WEST NI SHABIKI WA SIRI WA LIVERPOOL ??

Star wa wamerekani na mke wa kanye west Kim kardashian west, ameonekana kapost picha akiwa amepiga na rafiki yake huku nyuma yao kukiwa na picha ya Liverpool manager jurgen klopp , watu wengi wamejiuliza je Kim kardashian ni sgabi wa Liverpool inasemekana kwamba Kim kardashian ni shabiki wa kujificha wa klabu hiyo ya uiingereza ambayo kwa sasa imekua ikiinuka vizuri kuliko kipindi chake cha nyuma na ile khali  ya umoja na kujituma umeongezeka katika klabu hiyo.











Wednesday, May 11, 2016

RAISI MSTAAFU JK AMJIA JUU MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM NAKUMSHAURI AZINGATIE MIPANGO ILIYOWEKWA NA SERIKALI YAKE ILI AWEZE KUMALIZA MSONGAMANO WA MAGARI DAR. Endeleaaa....


jakaya Kikwete alitoa ushauri huo jana, alipotembelea Daraja la Nyerere, Kigamboni jijini Dar es Salaam, huku akionyesha kuridhishwa nalo na kumtaka Makonda kuweka historia kama mkuu wa mkoa kijana kumaliza msongamano.
Alisema kuna mipango ambayo iliwekwa na serikali ya awamu ya nne katika kumaliza msongamano huo, ikiwamo uboreshaji wa reli ili kubabiliana na tatizo la usafiri, uboreshaji wa stendi za mabasi ya kwenda mikoani za Boko, Pugu na Mbezi Luis, ambavyo alisema ni muda mrefu sasa haoni utekelezaji wake.
“Kwa mfano kuna ile stendi ya Boko na mingine ni mipango ambayo iliwekwa lakini naona imekaa muda mrefu hakuna utekelezaji wake. Naona tu unakwenda unarudi, unakwenda unarudi, ” alisema.
Kikwete alisema hakuna uchawi utakaosaidia kumaliza msongamano katika jiji la Dar es Salaam pasipo kuboresha huduma za msingi katika makazi yaliyoko pembezoni mwa mji huo pamoja kutumia treni.
Alisema jiji la Dar es Salaam linahitaji usafiri ambao utachukua idadi kubwa ya watu kwa wakati mmoja na kutolea mfano baadhi ya maeneo ya Ubungo, Tazara, na Mwembechai kwamba endapo yangewekwa reli na treni ikaanza kutumika, ingepunguza idadi ya magari binafsi barabarani.
Alisema pamoja na kuanza kwa mradi wa mabasi ya mwendo kasi, bado kunahitajika usafiri wa treni katika jiji, ambao alisema ukiboreshwa vizuri utawavutia hata wa wa maisha ya kawaida kuutumia na pia na kuacha magari yao nyumbani.
“Tatizo kubwa la Dar es Salaam wakazi wengi wanapata huduma katika eneo moja, yapo maeneo ya Mabwe Pande, Kigamboni na mengine ya pembezoni. Yatumieni vizuri, wekeni huduma huko, jengeni maduka, osifi na huduma muhimu huko. Sisemi mhamishie huko ofisi za serikali lakini huduma ziingine muhimu ili yule atakayetaka kuja mjini awe amependa mwenyewe,” alisema.
Makonda alisema amapokea ushauri huo na ataufanyia kazi na kuongeza kwamba iko mipango mbalimbali ambayo imeandaliwa kwa ajili ya kupunguza kero hizo 

Tuesday, May 10, 2016

Kiungo wa klabu ya benfica na timu ya taifa ya ureno, aliyekua akiwaniwa na klabu kubwa ikiwemo Manchester united na bayern munich sasa amewaziba midomo mashabiki na bodi ya ufundi ya Manchester united baada ya kujiunga rasmi na klabu ya nchini ujerumani bayern munich kwa euro 35m maelezo zaidi tembelea https://www.fcbayern.de/en/news/news/

 

Monday, May 9, 2016





















Kiungo mshambuliaji wa klabu ya juventus nchini italia Paul pogba anawindwa na club kubwa duniani, baadhi ya klabu hizo ni Barcelona na chelsea.
Karibu katika ukumbi wa habari za michezo aina yote, usisahau kua michezo huweka mwili katika hali salama ,kuongeza kinga ya mwili dhidi ya magonjwa hivyo tunaimizwa kufanya mazoezi na kula chakula chenye mpangilio mzuri wa virutubisho vyote.